Uhakiki wa Nafasi ya TEKNOHAMA katika Kukuza Maudhui katika Tamthilia ya Kigogo
Abstract
Fasihi ni zao la jamii na hubadilika kila uchao. Uwakilishi wa suala la
TEKNOHAMA katika tamthilia za kisasa umechukua mkondo mpya.
Hii ni kwa sababu, kutokana na jinsi dunia inavyobadilika ndivyo
masuala ya kiteknolojia pia yanavyoathiri fasihi ya sasa na
kuipa mguso
na taathira mpya. Licha ya uwakilishi wa TEKNOHAMA kuwa na
umuhimu katika kukuza fani na maudhui katika fasihi, mchango wake
katika tamthilia ya
Kigogo
haujafanyiwa utafiti, suala linalomchochea
mtafiti kulitafiti. Lengo kuu la utafiti huu ni
kutathmini mchango wa
TEKNOHAMA katika kukuza maudhui katika tamthilia ya
Kigogo
ya
Pauline Kea (2016). Utafiti huu unaongozwa na Nadharia ya Uhalisia.
Uteuzi wa sampuli utafanywa kimakusudi na utafiti wenyewe ni wa
muundo wa kiudhamano. Mtafiti atasoma ma
kala mbali mbali
kuhusiana na mada na kisha kuichanganua data kwa njia ya kimaelezo.